
SEHEMU YA 01 Mvua ndogo ndogo ilikuwa ikinyesha katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam huku watu wakikimbizana kutafuta hifadhi. Wengine waliingia kwenye maduka makubwa, wengine wakapanda magari yao ya kifahari na kuondoka kwa kasi. Lakini katikati ya barabara, kijana mmoja mwembamba aliyekuwa amevaa shati la zamani lililochanika mabegani aliendelea kutembea kana kwamba hakuhisi hata tone la mvua lililokuwa likimlowesha. Mgongoni alikuwa amebeba mfuko mkubwa uliojaa makopo ya soda na maji aliyokuwa ameyakusanya tangu asubuhi. Jina lake alikuwa Ayman. Alikuwa na miaka ishirini na miwili. Uso wake ulionekana kuchoka, lakini macho yake yalikuwa na utulivu wa ajabu. Utulivu wa
0 Comments