
SEHEMU YA 04 "Huu mnyororo ni wa chokoraa?" Zuhura alihisi kichefuchefu, akautupa ule mkufu mezani kana kwamba umeshika sumu. "Aisha, unamaanisha yule mchafu wa makopo anatembea na kitu cha dhahabu ya kale kama hii? Atakuwa ameiiba mahali! Lazima tuwaite polisi." "Hapana! Msithubutu!" Aisha aliuwahi ule mkufu na kuuficha viganjani mwake. Moyo wake ulikuwa ukidunda kwa kasi. Alitazama alama ile ya mwezi na nyota. Alijua fika kuwa baba yake, Mzee Salim, alikuwa na nembo kama hiyo kwenye pete yake ya ukoo, lakini mkufu huu ulionekana kuwa wa zamani zaidi na wenye thamani kubwa isiyoelezeka. "Mimi mwenyewe nitamrudishia." Aisha aliondoka pale mgahawani
0 Comments