
“Malaika! Malaika mwanangu!” “Naam mama... mbona unaniita kwa presha hivi, kuna nini tena?” Mama mkwe aliingia ndani huku uso umemshuka kama amekula ndimu, yaani kuanzia asubuhi alikuwa na jambo lake limekaa kooni. Miaka mitatu sasa imepita tangu Malaika aolewe na mwanawe kule Mwanza, lakini nyumba imepoa kama jokofu. Hakuna hata kichefuchefu cha uongo, wala tumbo kuchomoza—hakuna kitu kabisa! Na kwa mama mkwe, hili jambo lilikuwa linamfanya apandishe mori. “Malaika,” mama alianza kumpiga dongo, “hivi wewe kwenye hii nyumba ya mwanangu ni pambo la ndani au mke?” “Hapana mama,” Malaika alijibu kwa upole huku akitetemeka, maana alishajua tu hapa ni mwendo
0 Comments