
Sababu ni IPI? Wakati wa ujauzito, hutokea mabadiliko ya vichocheo (homoni), ambavyo baadhi husababisha kano (ligaments) za nyonga na kiuno kulegea na kujivuta ili kuiandaa nyonga kuzaa. Hali hiyo husababisha mkazo(strain) kwenye nyonga na kiuno, hivyo kusababisha maumivu. Pia uzito wa mtoto anayekua tumboni huongeza mkazo kwenye kiuno na nyonga na kusababisha MAUMIVU. UNAWEZAJE KUZUIA TATIZO HILI. 1. Jizuie kunyanyua vitu vizito ukiwa mjamzito, kama inakubidi kunyanyua , basi, chuchumaa, nyoosha mgongo, kaza nyonga na hakikisha mzigo upo karibu na mwili wako. 2. Pendelea kulala kwa kutumia ubavu, usilalie mgongo. Pia wakati wa kunyanyuka kitandani , nyanyuka kwa ubavu, tumia
0 Comments