
Basi Kutokana na jinsi kesi yangu ilivyokuwa kubwa, nilipigwa marufuku kukanyaga darasani. Nilipewa na adhabu ya kung’oa kisiki wakati nikisubiri mama afike kesho yake. Wakati nipo bize natokwa na jasho na maumivu ya kung’oa kile kisiki, Purity yeye alikuwa anadunda tena akila maisha kana kwamba hana hatia yoyote. Kibaya zaidi, yule mpuuzi Ticha Jembe alikuwa anajipitisha pale nilipokua nafanya adhabu akicheka huku akinambia "Mtoto mzuri pole kwa kupigwa na jua! Ungenipa aya yote yasingekukuta” Alijua kunikera yule baba acheni tu! Nilitamani niende kwa mkuu wa shule nikamuambie tabia zake sema ndo ivyo wasinge niamini maana ni mwalimu anae aminika sana💔.
0 Comments