
SAUTI YA KIMYA. SEHEMU YA 03. Mwandishi: Chief na simulizi zake WhatsApp:0621045997 Lile basi la Dar es Salaam lilitua stendi kuu likiwa limejaza vumbi la safari ndefu. Moyo wangu ulikwenda mbio niliposhuka na ule mfuko wangu mmoja wa nguo zilizochubuka. Jiji lilikuwa kubwa, la kelele, na lenye harakati za kutisha, lakini sikuwa na muda wa kushangaa maghorofa,fikra zangu zote zilikuwa chuo. Kufika chuoni, nilikabiliwa na ukuta mwingine mrefu usajili. Kwa kuwa nilichelewa kwa mwezi mzima, majina yangu yalionekana yameshafutwa kwenye mfumo wa awali. Ilinibidi nikimbizane kutoka ofisi moja ya utawala kwenda nyingine, nikiomba, nikieleza shida ya nyumbani, na kuonyesha ule
0 Comments