
Basi nikaanza kupapsa sasa macho yangu, mtu wa kwanza kukuona alikuwa ni mama yangu mzazi, na alikuwa amekaaa pembeni ya kitanda changu, basi mama alipoona nimefumbua macho haraka akanisogelea, akanishika mkono ,basi na mm nikataka kuinuka ila mama akanmbia hapana, hapana mwanangu usiinuke, apo nilikuwa nahisi mwili wangu ni mzito mnoo, yani kama.nimepewa mwili wa mtu, yani nilikuwa nahisi mwili umechoka sanaa, mama akanmbia ningoje nimuite daktari sawa, nikasema sawa ,basi mama alipotoka tu, akaingia baba, na ndugu zangu wotee, yani dada zangu wote walikuwa pale kumbe, nikajisikia farajaa mnooo kuwaona, na sisi ndo tupo hivyo baba katulea katika upendo
0 Comments