UTANIITA SHEMEJI* SEHEMU YA 10

UTANIITA SHEMEJI*  SEHEMU YA 10

SONGA NAYO................. Kauli ya ole wako uinuke na inuka zilikuwa nyingi hadi nikahisi kuchanganyikiwa ikawa ni mwendo wa simama kaa kama mtoto wachekechea . Mwisho Aunt Vero aliingilia kati na kusema " Dada!! Alvin yuko sahihi ,muache mtoto wawatu " Kauli ya aunt Vero ilimfanya madam akaachana na Alvin na kuhamia kwake, kwa hasira akamuuliza " Vero unasemaje!! Ina maana unamuunga mkono huyu mpuuzi?" "Sio kwamba namuunga mkono , sikia shoga angu Wardah bado ni mdogo mno hastahili kukaa kwenye nafasi unayotaka kumueweka " "Eti mdogo anaudogo gani huyu ,na kwanza yeye kuwa mdogo au mkubwa vinanihusu nini mimi? .

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments