
Macho ya Tahiya yalipofunguka na kukutana uso kwa uso na yule mlinzi aliyemshika kwa nguvu, moto mkubwa wa hasira ulichochewa ndani ya moyo wake. Alikuwa hajawahi kushikwa kwa dharau ya aina ile tangu azaliwe. Kila mwanaume aliyewahi kukatiza kwenye maisha yake alikuwa akipiga magoti, akitetemeka kwa hofu ya utajiri wake au akijipendekeza kwa sura yake nzuri. Lakini mwanaume huyu ambaye bado hakujua hata jina lake alikuwa akimnyanyasa mchana kweupe ndani ya nyumba yake mwenyewe. "Niachie mara moja!" Tahiya alifoka kwa sauti iliyojaa ukali na vilio vya hasira, akipiga teke kwa miguu yake iliyovaa viatu vya gharama huku akijaribu kujiengua kutoka
0 Comments