MY BODYGUARD 03

MY BODYGUARD 03

Taa zilizomulika eneo lile zilimfanya mtu yule aonekane wazi. Alikuwa ni mlinzi mmoja mrefu, mwenye mabega mapana na uso uliotulia bila kuonyesha woga wala tabasamu. Alikuwa amesimama akizuia mlango wa nyuma bila hata kutingisha mwili wake. Tahiya alifungua macho yake kwa mshangao mkubwa, kisha hasira zikapanda ghafla hadi kichwani mwake. Aliachia mbali ile tabasamu ya dhihaka aliyokuwa nayo awali, akaweka mikono yake kiunoni kwa maringo na kusogea hatua chache mbele huku Brenda akimfuata kwa nyuma huku akishangaa kwa uoga. "Wewe ni nani unayesimama hapa usiku wa manane bila ruhusa yangu? Toka kwenye njia yangu kabla sijakuita walinzi wakutose nje kama

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments