
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 15 Usiku ule uliofuata baada ya zile vurugu za kisaikolojia klabuni, Leon alirejea nyumbani kwake akiwa amechelewa sana. Mwili wake ulikuwa umechoka kupindukia, na akili yake ilikuwa imegawanyika vipande vipande. Alipofika kwenye chumba chake kikubwa cha kulala, alitupa funguo za gari kwenye meza ndogo iliyokuwa karibu na mlango, kisha alitembea kwa uzito kuelekea ukingoni mwa kitanda. Alikaa hapo huku akiwa bado amevaa nusu-suti yake iliyochoka, akianza kutafakari kwa kina na kwa ukali kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya moyo wake. Kichwa chake kilikuwa kizito, lakini jina pekee lililokuwa likijirudia
0 Comments