
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 25 Jonathan alimkodolea Nadia macho kwa sekunde kadhaa alipokuwa akipita kwa mbali, kisha akatikisa kichwa chake kwa dharau ya wazi na kuanza kumponda bila huruma yoyote. "Huyu? Aiseekakaangu, huyu binti anaonekana mshamba wa kutupa, hana kabisa hadhi ya kusimama karibu na mtu wa aina yako. Yaani mavazi yake ya kitenge na jinsi alivyo tu vinaonyesha kabisa anatoka familia ya chini, hana staili ya mjini wala mvuto wowote wa kiburudani tunaouzoea." Aliendelea kumtolea maneno ya kejeli na vijembe, akiamini alikuwa akiongea ukweli mtupu kwa mtazamo wake wa kijuujuu, bila
0 Comments