
Maria aliondoka na kwenda kuanza maisha mapya baada ya wiki moja kupita alirudi nyumbani kwakina Liya akachukuu vitu vyake . Liya alikuwa na wasiwasi juu ya urafiki wao alimuuliza " Maria umenikasirikia? Maria alitabasamu Kisha akasema " mjinga wewe kwanini nikukasirikie, wewe Ni zaidi ya rafiki imekuwa ndugu kwangu. " Lakini baba .... " Shiiii sitaki uongelee yaliyopita huenda baba yako alikuwa na maana alipotaka niondoke. Umeona Sasa hivi nimeanza kujitegemea pia akili ya kutafuta kazi ilikuja haraka hivyo baba alinitakia mema. Liya alimsogelea akamkumbatia " Daima nipo pamoja na wewe ukiwa na tatizo niambie alafu nahitaji kupafahamu unapoishi. "
0 Comments