
By Simulizi za john 0789 824 178 Mmhhh nikashangaa kuumwa😪ile nataka kukataa ghafla nikasikia sauti ya Bill ananiambia dawa hizi hapa mke wangu nimekuletea na zawadi yako pia.. Niligeuka kwa mshangao nikakutana na Bill uso kwa uso nilionyesha tabasamu la kinafiki nikampokea mume wangu kwa mahaba watu wakabaki wanatabasamu tu.. Asante mume wangu❤️naye akasema it's okay baby twende chumbani chakula chako nitakuletea hukohuko.. Basi alinishika mkono tukaelekea zetu chumbani.. nilivofika chumbani nikabadili sura😔nikanuna nikaweka vile vitu kitandani nikageukia upande wa pili.. Bill alinikumbatia kwa nyuma akaniambia sorry najua umekasirika kwa sababu nimeongea uongo mke wangu.. Kumbe unajua?? Mimi nilitarajia utamwambia
0 Comments