
By Babie LOve Lakini Paris hakuna chochote inamaana huniamini?? Ndio sikuamini tena sikuamini kwa asilimia miamoja😪ukitaka nikuamini nitolee hii simu lock sasa hivi.. Okay fine alitoa lock akanipatia simu alikuwa na presha mpaka jasho lilianza kumtoka.. Mimi mwenyewe mapigo ya moyo yalikuwa yananienda mbio si kawaida😪nilijiuliza kwenye hii simu kuna usalama kweli?? Mbona moyo unanienda mbio sana😪lakini acha tu niikague nijue mapema kinachoendelea.. Nilienda upande wa msg nikaanza kusoma msg za Morgan na Bill Bill alishindwa kukaa pale chumbani akaamka na kutoka nje😪nilisoma msg moja baada ya nyingine.. Aisee marafiki wa kiume nao ni mbwa kumbe😏imajini Morgan alikuwa anamshauri Bill
0 Comments