
PART 1; CHOZI LA BINTI MASIKINI Mtunzi: Lipeta S Shaaban Asubuhi Katikati ya jiji la waswahili wanapoishi waswahili, wao wanapaita uswahilini. Kelele za ndege aina ya kunguru zinasikika. Giza lilikuwa linatokomea taratibu na mwangaza wa jua la asubuhi likitaradi. Chumbani kwenye nyumba moja iliyochakaa, Bibi Zena akiwa bado yupo kitandani alichukua simu yake iliyokuwa kitandani na kuiwasha. "Saa kumi na mbili na dakika kumi!" Alisikika akizungumza Bibi Zena kwa mshangao mithili ya mtu aliyeshika butwaa. "Nililala saa ngapi sijui" Alijiuliza mwenyewe pasipo kujijibu. Aliamka toka kitandani na kwenda hadi sebuleni kwake ambapo meza kubwa chakavu pamoja na viti vichache vya
0 Comments