
Alivyotoka tu mimi mbio kufunga funga milango, kesho yake ilikuwa jumamosi, niliamua kufanya fanya usafi nyumbani, nilivyomaliza nikatoka kwenda kuosha nywele ndo nikakumbuka yaliyonitokea jana, ila sasa kimbembe sehemu kubwa nikawa nakumbuka tu mambo ya kijinga... Nilienda kuosha nywele, lakini sikusuka, nilifunga zangu mchicha, uyo nikaenda kuhemea chakula na mahitaji ya nyumbani kwangu, sikuisahau laki, ila kadi sikubeba kabisa, nilijua tu, huyu mwanafunzi hana pesa, amedunduliza za kuomba omba na kudanganya kwa wazazi ndo kaamua anipe mimi... Nilienda duka ninalochukulia vitu nakuta nimeshalipiwa tena zaidi ya ninavyochukua, niliuliza nani kanilipia, nijahisi huenda mlokole wangu kaludisha moyo nyuma, lakini hakuwa akinihudumia
0 Comments