
ENDELEA..... Niliendelea kuzunguka mule chumbani nisielewe nini nifanye. Nilisogelea dirisha na kuchungulia Kwa nje. Kwa macho yangu nilimuona Jafari nje ya geti amesimama. Jafari alitazama juu na kuniona pia. Alinipungia mkono na baada ya hapo aliongea Kwa ishara kwamba muda alionipa unakaribia Hana masihara ataingia kweli. Nilizidi kuchanganyikiwa. Niliaangalia saa kwenye simu yangu ilikuwa ni saa kumi na mbili kasoro jioni. Ni muda wa mume wangu kuludi. Nilimtazama Tena Jafari niliona anasogelea geti taratibu huku ananitazama. Nilimpigia simu alipokea. "Tafadhali usiingie natoka Mimi". Niliyasema hayo na kukata simu. Nilitoka chumbani kwangu kwa kuibia sikutaka mtu anione kama natoka nje. Nilikuwa
0 Comments