
Sehemu ya kumi na moja ENDELEA....... Siku iliyofuatia Catarina alimpigia simu David "Njoo ghetoni kwangu kuna kitu nataka unisaidie" Wacha David apaliwe mate baada ya kusikia kuna kitu anatakiwa kwenda kutoa msaada "Huu si mtego jamani, nishaelewa ni kitu gani Catarina anataka. George kanizidi pesa tu ila kimuonekano nimemuacha mbali sana.....wacha niende kuichapa" David alijikuta akiwaza vingine kabisa Alivunja kabati kwa kutupia code matata. Vivi na George walibaki kutazamana "Nini kimetokea, mbona leo umependeza namna hiyo 🙄" George aliuliza David akiwa anajichekesha" Naenda kanisani...." "Ooh sawa, hivi Catarina amekupigia simu? maana namtafuta hapatikani na Ofisini kwake nasikia hajafika" George aliuliza
0 Comments