
BINTI MIA Mtunzi: Chief na simulizi zake WhatsApp: 0621045997 Sehemu ya 16 Nilimwambia Eva kila kitu naye akaniambia kubwa hapo mtihani mkubwa, maana kutoa hiyo mimba ni dhambi pia nikizaa ndipo pengine litakuwa tatizo kubwa maana hapo shemeji ataendelea tu kunisumbua kivyovyote. Aliniambia nitulize kichwa kwanza naye anatafuta ushauri mzuri sana. Nilimshukuru sana na kumuomba hiyo siri asimwambie mtu maana dah! Sijihisi amani kabisa, akanambia nisijali kabisa yeye ndio mficha siri zangu. Ilipita wiki mbili nikiwa sina raha hadi Victor akawa ana wasiwasi kuwa nina nini, au amejisikia vibaya baada ya kuniambia mbona nimebeba mimba bila kukubaliana! Nilimtoa wasiwasi tu
0 Comments