
GANGSTER IN LOVE Sehemu ya 7 Nilitoka haraka huku ninakimbia kumuwahi John. Akili yangu ilikua na amani sanaa kwamba tunaenda kuyamaliza na John. Nilimkuta John amesimama, uso wake umekunjamana kama mtu mwenye hasira sana. "Samahani nimechelewa kidogo," nilikua najichekesha chekesha huku nabinya binya vidole vyangu. John hakuonesha kabisa kuvutiwa na mimi kuwa pale. "Hivii we Sintya unaakili?" Bila hata kunijibu wala salama, nilishangaa anaanza kufoka kwa sauti mpaka watu wa pembeni walianza kutuangalia tulipo kuwa tumesimama. "Nimefanya nini John? Ongea basi taratibu, watu wote wanatutazama sisi ujue." Nilikua nikiongea kwa sauti ya chini kabisa ili kumshawishi. "Tena usinipangie, umenisikia wewe?
0 Comments