
Kulikucha ilikuwa majira ya saa moja asubuhi Lena alikuwa amekaa kitandani kwake na kichwani kwake alikuwa na mawazo mengi sana ukizingatia Aron hakurudi nyumbani na hakujua yuko wapi. Alichukua simu yake iliyokuwa pembeni akapiga namba ya Aron. Simu ya Aron iliita maramoja na kupokelewa. Simu ilipokelewa lakini hakuongea chochote. " Aron mume wangu uko wapi? Aliuliza Lena lakini hakujibiwa. " Aron naongea na wewe acha kunipa wasiwasi mwenzio . Jana umeondoka ukumbini ghafla tena hukuniambua unaenda wapi . Ghafla akasikia sauti ya kike. " Mume wako yuko bafuni anaoga. Moyo wa Lena ulipasuka kwa wivu. " Wewe nani ? "
0 Comments