
LIAM alikuwa kama hajaelewa alichoambiwa. " Unasemaje wewe? " Lola ni mtoto wako wa kumzaa mishipa ya Lola unapitisha damu yako. " Si wewe ulisema kwa kinywa chako kuwa Lola ni mtoto wa Aron? " Nikisema lakini nilidanganya. " Sasa tutajua mimi vipi? Maya aliuliza " Kipimo cha dna. LIAM alikuwa haamini alihisi Lena anamtania. " LIAM nataka umlee mtoto wako . " Siwezi kukubali kirahisi nataka tufanye kipimo cha dna. " Sawa, tufanye kesho kama hutojali. " Sawa. Baada ya maongezi Lena aliondoka. Kesho yake mapema sana Lena alienda hospitali na mtoto wake. LIAM na Maya pia walifika .
0 Comments