
Mwandishi: Kitty Fefe Naitwa Radhia...nilizaliwa mimi na dada yangu Rehema, ila hatujawahi kumwona baba yetu hata siku moja. Mama anasema aliondoka muda mrefu kabla hata sijajua kuhesabu umri wangu. Ndio maana mama amekuwa kila kitu kwetu, baba na mama kwa pamoja.Nyumba tunayokaa ni ya urithi. Imejengwa na bibi na babu yetu zamani, ni ya matofali ya kuchoma na bati zake zimeshachakaa,Ni nyumba ya familia ambayo haijawahi kufungwa mlango kwa funguo, maana kila mtu anaingia muda atakao yeye.Tunaishi pamoja na mjomba wangu, ni mlevi sana yeye ndiye mtoto wa kwanza wa bibi na babu. Ana mke wake ambaye yeye anajishughulisha na
0 Comments