
ME AND YOU Sehemu ya 5 Maskini alikuwa mlemavu! Na ndio mtoto wa pekee wa Stephano. "Haya! Tusipoteze muda! Mimi kwangu sitaki utani na wafanyakazi kabisa, hujui kilichokuleta hapa, mlango upo wazi unaweza kuondoka. Sipendi watu wavivu, unajua huwezi pilika pilika za humu ndani? Again, mlango upo wazi unaweza kuondoka! Kingine hapa mmekuja kama team, akikosea mmoja mnaondoka wote! Sijui mnaelewa….?" Mama mwenye nyumba alitaka kuhakikisha kama tuna uelewa moto wake. "Ndio Madam…" tulitikia kwa pamoja. "Ndani kwangu siruhusu mahusiano! Nikijua baadhi yenu mmekuja kwa ajili ya mahusiano na sio kufanya kazi, nafukuza wote!……" Hilo onyo nahisi lilikuwa langu maana
0 Comments