
🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋🦋 Robert hakusubiri hata zege lilale! Alimfuata Margarita ofisini kwake usiku wa siku hiyo. “kuna kitu nataka kukuambia” alisema. “Kitu gani tena?” Margarita akanyanyua macho kutoka kwenye laptop yake. “Nikikuambia… utanisaidia kupata ninachokitaka?” “Unataka nini?”🤔 “Namtaka Eve” Kusikia vile Margarita akaanza kucheka sana mpaka akashika tumbo. “Nilijua tu!” alisema huku bado anacheka “nilijua unampenda yule binti maana sio jinsi unavyo mtazama! Na nimegundua kuwa unaona wivu anapokua busy na Dalton…. “ “Utanisaidia?”🤷♀️ “Na ukisaidiwa utanifanyia nini!!! Na utampataje Eve???” “Dalton lazima aondoke hapa” Robert akasema. “Bila hivyo sitaweza kumpata Eve” “Dalton kuondoka hapa si rahisi, unajua kabisa siwezi kuruhusu ilo”
0 Comments