
ENDELEA....... Jafari aliinamisha kichwa chini Kwa uoga ujanja wote mfukoni. "Kaka nisamehe". Alianza kuomba msamaha Kwa sura ya huruma unaweza sema sio yeye vile". "Nikusamehe Kwa kosa gani?". Samir alimuuliza Jafari. Jafari alibaki kimya. "Shuka kwenye gari". Samir alimwambia Jafari kwa sauti ya mkazo. Jafari hakuwa na jinsi zaidi ya kushuka kwenye gari. "Njoo nifuate". Samir alimwambia Jafari. Wee Jafari alivyoambiwa nifuate akavizia kutaka kukimbia ila kabda hajafanya hivyo Samir alimshika mkono Kwa nguvu. "Kaka unataka kunifanyaje, naomba unisamehe sitoludia Tena". Jafari aliendelea kuomba msamaha japo hakujua amefanya nini. Samir alisimama na kumgeukia Jafari. Alimuangalia Kwa sekunde kadhaa alafu alimuuliza.
0 Comments