
...... ENDELEA... Upande wangu nilifurahi, hakuna mwanamke anapenda uke wenza. Nisiwe mnafki baada ya Samir kusema anataka kumuacha mwanamiss nilifurahi moyoni. Samir alichukua simu yake na kumpigia Jafari. Jafari hakupokea simu. Alipiga kama mala tatu pasipo Jafari kupokea simu. Samir alimtumia ujumbe Jafari. "Unajifanya mjanja?, mimi kukupata wewe ni dakika Moja tu. Nakwambia utakapofika Tena mikononi mwangu utajuta maisha Yako yote". Ujumbe wa Samir ulifika. Jafari hakujibu na kwauoga alichomoa line Yale kwenye simu aliitupa kabisa asipatikane Tena. Alihofia huenda Samir angemtafuta kupitia ku track namba na ungekuwa rahisi kumpata. "Baada ya wiki moja kupita tangu Jafari aje nyumbani kwangu
0 Comments