
Wakati anaingia bafuni Bastola alikua kaishika kwa nyuma ivyo sikuiona! Aliingia spidi akakuta nipo mwisho kabisa wa bafu nimejibana ukutani nikiwa kama nilivyo zaliwa. Aliangalia kulia na kushoto kwa umakini, kisha akauliza, "Vipi? Kuna nini?!" "Nimeona kitu!" nilijibu kwa sauti ya kutetemeka. "Kitu gani?!" "Mende..." nilijibu kwa upole🥹. Jamaa kwanza akashusha presha, akatulia kwa sekunde kadhaa ndipo Akili yake ikarudi sawa na kuniangalia kuanzia juu mpaka chini. Kama mwanaume lazima ajihisi tofauti kuniona vile! Nilitegemea angefanya kitu ila cha kushangaza alitoka kimya kama hajaona chochote. Nilichukia sababu mpango ulifeli! Nikasema usinitanie lazima nikamilishe mpango wangu! Nikajifunga kanga nikamfuata sebuleni haraka
0 Comments