
Nyuma ya kabati lake niliona kama kuna taa inawaka! Kihere here changu na umbea wangu nikaenda kuangalia. Kuchungulia nikaona taa inawaka ila sikuona vizuri. Nikasogeza kabati kidogo ndo nikashuhudia vitu ambavyo sikupaswa kuona. Jamaa alikua katengeneza safe ukutani kapanga silaha kuanzia juu mpaka chini! Kuna mabomu na visu vya kila size. Nyiee Nilishtuka nikabaki nimeganda😳. Nilianza kutetemeka na kujiuliza nimejiingiza kwenye nini! Zile silaha niza nini? Au ni jambaazi??? Ndo maana kazi zake niza usiku! Ndo maana anaishi kujificha ficha. Nilihisi kuzimia…pumzi ikawa inakata kata! Nikagundua pale sio salama kwangu anaweza hata kuniua. Nikasogeza kabati kama nilivyo likuta kisha nikatoka
0 Comments