
SEHEMU 06 Ilipoishia...... Niliachia tabasamu kimtindo. Muda huo huo mama mkwe wangu alikuja chumbani. "Nimekuletea dawa uanze kutumia.Hii dawa ni nzuri sana kama utaitumia kwa ufasaha na ukaweka imani nayo. Wanawake wengi waliokuwa na tatizo kama lako walipata furaha baada ya kutumia hii dawa. Ni dawa ya asili uliyotengenezwa na miti shamba" Mama mkwe alitueleza kwa urefu ili kutuondoa hofu.............. Endelea....... Nilipokea kikombe cha dawa. "Msimamie anywe hiyo dawa yote" alimwambia mume wangu. Alitoka chumbani Sam akinibembeleza ninywe dawa aliyoniandalia mama yake. "Nina uhakika hata Sam haitaji nimzalie. Mimi sio mwanamke wa ndoa zake ni mwanamke wa malengo yake tu.
0 Comments