
Tulipoishia... Siku moja jioni nilipotoka chuo wakati narudi nyumbani niliikuta gari ya saji ikiwa imepark nje ya nyumba yangu.. Alikuwaga na kawaida ya kuwa anakuja kututembelea mara kwa mara lakini siku hiyo alikuja kivingine sio kama nilivomzoea.. Siku hiyo saji alikuja na kila kitu chake akahamishia pale kwangu alihamisha kila kitu chake kutoka kule alipokuwa anakaa na mke wake Maria akaleta huku kwangu... Nilishangaa baada ya kumuona na mizigo nilimsogelea huku nikimuuliza kulikoni mbona na mabegi?? Saji aliniangalia lakini hakunijibu kitu alifungua mlango wa gari langu akamshusha mwanangu kassy alimkumbatia kwa zaidi ya dakika tano.. Baada ya hapo aliomba nifungue
0 Comments