
SAUTI YA KIMYA SEHEMU YA 02 Ahadi ya kwenda Dar es Salaam ilianza kufifia mbele ya ukuta mrefu wa umaskini. Lile neno "nauli na mahitaji" halikuwa neno tu kwenye karatasi ya kujiunga na chuo (joining instruction) lilikuwa donda ndugu lililoanza kuinyima usingizi familia ya Mzee Shirima. Baada ya shangwe za matokeo kuisha, mtaa ulirudi kwenye ukimya wake, na ukweli mchungu ukabaki sebuleni kwetu. Siku zilizofuata ziligeuka kuwa za mapambano ya kufa na kupona. Kila asubuhi ilianza kabla ya jua kuchomoza. Mzee Shirima, ambaye mgongo wake ulikuwa umeanza kuinama kwa miaka mingi ya kazi ngumu ya sulubu, aliongeza masaa ya kufanya
0 Comments