VICK 01&02

VICK 01&02

VICK 01 SEHEMU YA KWANZA Ilikuwa siku ya Jumamosi. Kuanzia asubuhi sikupata mteja hata mmoja, njaa ilikuwa inaniumiza kwelikweli. Nilikaa kwenye kachochoro fulani, nikapaki gari pembeni na kuwasha redio kusikiliza mechi ya Simba na Yanga ili angalau niliwaze akili na kusahau njaa hiyo. Nikiwa bado ninafuatilia mpira, nilipokea simu kutoka kwa mteja wangu mmoja wa nguvu—yule ambaye kila akipanda hutoa noti nyekundu tu na chenji haniachia. Nilifurahi na kupokea haraka sana. "Vick, hebu nenda haraka maeneo ya Kinondoni kuna mteja anataka taksi, fanya chapchap." "Yukoje huyo mteja?" nilimuuliza. "Ni mrefu, mweusi... mambo mengi siyajui bwana, ngoja nikurushie namba yake ya

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments