
01. Sikuwahi kufikiria wala kuwaza kama kuna siku nitakuja kumchukia kwango cha kumlaani marehemu kaka yangu na Mkewe. Kiufupi, nawachukia sana, yeye marehemu kaka na bibi harusi wake, nawachukia sana, tena sana. Popotea ulipo marehemu Kaka Fred, iwe motoni au peponi, naomba ujue nakuchukia sana, wewe na bibi harusi wako.Wote wawili nawachukia sana, na mlaaniniwe ile laana ya nguruwe . Naomba ungana nami kwenye hii simulizi kujua lipi ni lipi. SEHEMU YA KWANZA. Sikuwa tayari kuona Kaka yangu, Fred , akizikwa kwenye lile kaburi. Nilimfata baba na kumnongoneza. Baba aliniangalia kama mtu niliyechanganyikiwa. Aliyashangaa maneno yangu. “ Hutaki azikwe kwenye
0 Comments