
Safari ikawa inajitokeza na njiani kulikuwa na raha; mambo yalikuwa mengi ya kushangaza, mazingira mazuri yalinoga sana, na kila mtu alikuwa akipiga picha kivyake. Tukahama ule upande tukaenda upande mwingine wakati bado tuko ndani ya boti, tunajisnap sio poa. Kwa mbali nikamuona Karim ana kamera ya kawaida yupo anapiga picha na yule rafiki yake. Tukafika mwisho wa safari, waooh! Palikuwa pazuri jamani, mazingira yametulia, miti ya kijani, na fukwe inavutia hatari. Tulishuka wote, kiongozi mbele anatuongoza akiwa pamoja na wale wanaoongoza watalii. Tulitembea sehemu nyingi yaani na kote kulikuwa kutamu. Mwisho tulifika pale kwenye maji yanaporomoka, mengine tuliambiwa yanashika njia
0 Comments