
Basi akanambia, "Salma, naomba tukae hapa chini tafadhali." Alinambia huku ananikalisha kwa kushika mabega yangu, nilijikuta naketi tu. Na yeye aliketi pembeni yangu akawa amenishika mikono yote miwili huku ananitazama usoni. "Salma ongea basi, sema kitu kipenzi," anaongea huku anaipapasa mikono yangu, niko tu mmmh, mhh, mh. Sasa nitaongea nini? "Nitazame hata eeh," akaniinua kidevu kwa mkono mmoja. Heee! Niliweza hata kumtazama, nikakwepesha macho nikatazama kuleee. Sasa kama Mungu, yaani ile natazama hivi kwa mbali, si nikamuona Eliza yuko na Samson! Wee, niliinuka haraka. Karim akaniuliza vipi, nikamwambia, "Wanakuja watu," huku natimua mbio kuzunguka ile miamba. Nilipenyapenya nikarudi kule kule
0 Comments