
Mimi tena hapo nasikia raha, nasikia raha mpaka imepitiliza yaani. Tulitembea kidogo akanambia subiri hapo, nikasimama. Azunguka kwa nyuma yangu, yaani akawa amekaa mgongoni kwangu, akanambia nifumbe macho mi nikafunga bila shida. Akachukua kitambaa na kufunga macho yangu. Alianza kunitembeza taratibu ameshika mkono wangu mmoja, haya mambo mimi sijazoea kabisa, nilikuwa naona aibu lakini nimejikaza sana. Alinambia sasa hivi tumefika ziwani, kuwa makini kidogo unapotembea. Baada ya hatua mbili kweli nilikanyaga maji. Akanambia haya panda humo, nilipanda kwenye kitu nilihisi tu ni mtumbwi ule. Akaanza kupiga kasia huku bado ameniweka kitambaa bado machoni kwahiyo sioni. Baada ya muda alinifungua kile
0 Comments