
Nilikuwa kimya kumsikiliza huyo baba ambaye ni dereva kama alivyojitambulisha kwangu. "Bint, Eze amenieleza tayari kuwa amekwambia kuhusu maisha ya karimu si ndio?" Eze ndio yule kaka ambaye ni rafiki wa karimu kwa madai yake tangu wakiwa shule ya msingi lakini Karim mie hajawahi kumuongelea huyu kwa lolote hata kumtaja kwa bahati mbaya tu. Nilijibu, "Ndio!" "Nina ombi juu yako madam." "Nambia ninasikia." "Baba yake karim ni mgonjwa sana ni mgonjwa hoi yupo kitandani tangu ameumwa karim hajawahi kumuona hata kwa mbali, tamanio la yule baba ni kumuona mtoto wake wa pekee karim kitu ambacho kimeshindikana, nakuomba walau twende ukamsikilize
0 Comments