
Yule mama akaulizia nyaraka hata sijui nyaraka gani, mie nilikumbuka maelezo kabla baba mkwe hajajibu, niliaga fasta nikasema Uncle mie naenda mana kuna sehemu nina wahii. Alikubali akashukuru sana mie kwenda kumuona, nikaondoka na yule dereva, alinirudisha chuo, akaondoka zake. Hiyo siku sikuwa hata na raha, nilikuwa nawaza hapa lazima karim aende kwao lazima aonane na baba yake, lakini nitaanzia wapi? Mana yeye hajawahi niambia kama anashida na baba yake au kwao kuna matatizo! Sasa nitamuanza vipii? Lakini yule mama ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kumuona aisee huwezi amini nilimchukua! Yaani kila ikija sura yake ninasinyaa, yaani ni kweli
0 Comments