
Nilimuomba karim nami nina jambo langu nataka niongee nae akasema sasa hivi nipo huru kwako ila ngoja kwanza mpaka nije kuchukua majibu kabisa nikasema sawa. Jumatano bwana ilifika nakumbuka baba aliniuliza kuhusu kuolewa nikasema mie nipo tayari, akasema sio mpaka umalize chuoo? Nikasema mbali sana huko baba akanambia wafadhili watavunja mkataba nawewe kama wakijua umeolewa mmh nilibaki kimyaa hilo nalo tatizo. Walikuja kina karim kuchukua majibu yao hiyo siku vilikuwa havikaliki jamani, waliambiwa maombi yao yamekubaliwa kabisa, nilikuwa mlangoni nimetega sikio kwa makini sitaki kuhadisiwa. Walitajiwa mahali eti baba akasema laki saba haa karim kwao wanamahela hivyooo afu mi bikraa
0 Comments