A TOUR TO REMEMBER 33

A TOUR TO REMEMBER 33

Nilirushwa mbali na pikipiki kule. Niliona kama roho inaenda kuacha mwili. Kwa mbali nilimwona mtu anashuka kwenye ile gari, mpaka nilipokuwa alikuwa ni mwanaume lakini sikumjua. Pochi yangu ilikuwa imeanguka sio mbali na mie, akachukua akamwaga kila kitu ni kama kuna kitu alikuwa anatafuta. Hapo ndo na mie nilishangaa baada ya kuona, sikubeba pochi yangu ilikuwa pochi ya Eliza ile. Aliitupa chini akageuka kwangu aliniinamia akanambia kama hutaki kufa nambie karatasi zipo wapi? Nilipata presha nyie, kufa tena. Nikakata moto hapo hapo, hata sijui nini kiliendelea. Nilikuja kuamka nipo hospitali, nakumbuka mtu wa kwanza kumuona ni karim alikuwa pembeni yangu.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments