
Nilikuja kushtuka tayari umetengwa msiba wa bibi yangu. Ilikuwa asubuhi tena nipo chumbani nilipokuwa nalala na bibi. Niliamka nikatoka sebuleni, kulikuwa na minong'ono ya watu. Baada ya kutoka nasikia Mama Frank anawaambia, "Huyo ndo mjukuu wake, mimi niliwasaidia tu hapa tumsaidie tu kumzika bibi yake." Sikuamini bibi yangu hayupo tena. Sikuamini mimi ndo nimekuwa chanzo cha kifo cha bibi yangu. Nililia sana. Nililia nikiona kama niko kwenye shimo kubwa jeusi, shimo ambalo siwezi kufurukuta ndani yake. Nitaishi vipi mimi bila bibi yangu jamani? Mbona Mungu mimi hanipendi? Mbona amenisahau mimi na bibi yangu, kwanini?? Bibi yangu ameteseka mpaka siku anakufa,
0 Comments