
......nilikumbuka mengi sana kumuhusu bibi yangu kuanzia Arusha mpaka nilipopata upofu, shida nilizopitia hata kubakwa. Nilikumbuka kifo cha bibi yangu kilikatishwa na mpuuzi mmoja. Nilijikuta namlaani Frank na familia yake yote. Bila yeye huenda leo ningekuwa hapa na bibi yangu tunapata upepo mzuri kwenye jumba kubwa kama hili. Mpaka leo kuwa hai sio ujanja wangu, Mungu tu kanilinda sana. Sikuwa na budi kumshukuru na kumuombea bibi yangu apumzike kwa amani alipo. Usingizi ulinipitia baada ya mawazo mengi kunielemea. Kuna muda nilikuwa nawaza nini haswa sababu ya mama na Baba Sadru kunisaidia mimi. Ni kweli sababu nimefanana umri na binti yao??
0 Comments