MREMBO KIPOFU 11

MREMBO KIPOFU 11

Manka aliongea kama mtu mwenye uhakika na jambo lake kweli kweli, nikawaza au kuna maneno ameshamjaza mama kule? Mama ana mpango wa kunifukuza hapa, yaani nilikuwa nawaza kweli. Basi chakula kikapakuliwa bwana. Tonge moja tu la mama alikitema chakula chote. "Upuuzi gani huu?!" alifatisha na swali, likafuata la manka. "Jamaniii," sasa nikawa najiuliza nini, nikaganda na kijiko changu. Mama ananambia, "Kula au unajua ulichokifanya?" Nikaweka mdomon, salaleee! Chakula hata ulimini hakikai jamani, sijui ni uvinza imehamia kwenye poti la chakula. Mi mwenyewe nilikitema maana ni kama ulimi unakatika, chumvi kama vile iliwekwa pakti nzima. "Bianca mpaka hapo hujui kuweka chumvi??

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments