MREMBO KIPOFU 14

MREMBO KIPOFU 14

Nilipiga magoti pale muda mrefu sana, akili yangu ilikuwa imehama ndipo nilishtuliwa na mlango unafungwa. Haa, nikakumbuka Manka hakutoka pamoja na mama, lakini niliachana nae nilipanda kitandani nikajilaza. Natamani bibi aje nimuelezee, hata mimi sikuiba hela yeye anaweza kuniamini. Huyu mama alinipenda sana lakini, ameshindwa kuniamini... Usingizi ulinipitia ile jioni, nilikuja kushtuka usiku nilihisi homa kali mno. Kichwa kilikuwa kizito, akili yangu hata haifanyi kazi, maneno ya mama yalikuwa yanajirudia rudia kichwani mwangu. Maskini wala sikumlaumu mama, ila Manka, kila jina hili lilipokuwa linapita kichwani nilihisi kunipa ukichaa. Nilijifikiria tangu nimjue mpaka hapa, kuna kitu gani niliwahi kumkosea huyu msichana

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments