
Ilipita wiki moja lakini kaka hakurejea, yaani hapo Manka alikuwa ndie kama mtoto na mimi ndio kijakazi nyumbani. Mama alikuwa anarudi usiku sana nyumbani na akifika ni kuingia tu ndani kulala. Nafasi hiyo aliitumia vizuri sana Manka kuhakikisha ananishurutisha, yaani nililiwa nikisema hata nimechoka, mama akirudi tu anapewa mashtaka yangu kama yote na alikuwa anaweza kuweka mambo hata siyajui. Mama alikuwa anaongea kwa kufoka sana anasema, "Bianca nionee huruma basi nachoka nachoka Bianca nachokaaa!!" Kauli zilizokuwa zinaniuma mno. Nikisema mama sio kweli, ananiambia kuwa ni kawaida yangu kukataa makosa, sijawahi kukubali makosa yangu. Ili kuepuka kumchosha mama angu niliona wacha
0 Comments