
Baba alinitazama kwa muda nami nilimkazia macho wala sikupepesa. "Bianca embu nenda moja kwa moja binti yangu unatuchanganya," mama alisema huku akinitazama kwa macho yaani kama mtu mwenye hamu ya kujua. "Ni vyema ikawa hivyo naomba unikumbushe," baba alikandamizia. "Ni miaka mingi sana imepita ile siku ulipomuacha yule mtoto aliyepata ajali ya gari wodini na kuahidi kuwa utarudi kwa ajili yake kumfanyia matibabu huyo mtoto ulimpa upofu ndio mimi baba, Hukurudi tena, sura yako sijawahi kuisahau hata siku moja kwenye giza ni sura yako pekee ndie ilikuwa na nuru hata nilipo lala niliiona," niliongea kwa uchungu sana laiti asingekuwa baba
0 Comments