
Muda ulikuwa unayoyoma kuelekea saa tatu za usiku, na ndani ya chumba cha kifahari cha Tahiya, hali ya hewa ilikuwa imetawaliwa na harufu nzuri ya marashi ya bei ghali ya Baccarat Rouge, moshi mwepesi wa uvumba mtamu uliotoka kwenye chombo cha kuchomea cha shaba, na sauti za chini za muziki wa R&B uliokuwa ukisikika kupitia spika za ukutani za chumbani kwake. Tahiya alikuwa ameketi mbele ya meza yake kubwa ya kujipodoa iliyozungukwa na taa za kung'aa za vioo vya Hollywood, akijipaka rangi nyekundu ya midomoni huku akijitazama kwa kiburi kwenye kioo kikubwa. Kando yake, Brenda alikuwa amejilaza kwa kujitanua kwenye
0 Comments