
THE LOVE HE NEVER PLANNED Mwandishi: Chieff Stories Mawasiliano: 0621045997 SEHEMU YA 13 Baada ya kumalizika kwa ile presentation iliyovuta hisia za wengi, Leon alijipata akijivuta taratibu kuelekea nje ya ule ukumbi mkubwa huku akisindikizwa na pongezi kutoka kwa wanafunzi mbalimbali. Ingawa alionekana mwenye furaha kwa mafanikio ya kazi yake ya ualimu wa ghafla, akili yake ilikuwa imekwama mahali pamoja; haikuweza kutoka kwenye sura na ile sauti ya Nadia, msichana yule wa mwaka wa kwanza aliyevaa kitenge na kunyoa kipara safi. Wakati akisimama chini ya mti mkubwa uliokuwa nje ya ukumbi huo akipunga upepo ili kutuliza mawazo yake yaliyokuwa yanapambana
0 Comments